Sunday, 5 June 2016

JOB VACANCY IN ACCOUNT ASSISTANCE AT TGS C,


Mhasibu Msaidizi TGS C, Nafasi 3

Tume ya Utumishi wa Mahakama

Date Posted: Jun 4, 2016
Application Deadline: Jun 15, 2016
Position Description:
Source:Guardian,2nd June 2016
Tume ya Utumishi wa Mahakama nichombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka '1977. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada rnbalirnbali wa Mahakama.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi kwenye kituo chochote Tanzania Bara, katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko katika Mikoa na Wilaya mbalhnbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni
Tafadhali soma kwa makini na kuzingatia maelekezo vote yaliyoorodheshwa katika sehemu ya kumi na sita ya tangazo hili.
Mhasibu Msaidizi TGS C, Nafasi 3
Sifa
Kuajiriwa wenye cheti cha ufaulu mtihani mgumu wa Uhasibu Serikalini (Higher Standard Govemment Accountancy Examination) unaotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma au
Wenye Stashahada ya Kawaida ya Uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali. Aidha mwenye uzoefu usiopungua mwaka mmoja (1) katika fani hiyo atafikiriwa kwanza.

Kazi za kufanya:-
(i) Kupokea na kulipa fedha
(ii) Kutunza daftari la fedha
(iii) Kufanya usuluhisho wa hesabu za benki
(iv) Kukagua hati za malipo
(v) Kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha
(vi) Kusimamia kazi za Wasaidizi wa Hesabu.
Barua za maombi ziandikwe kwa. mkono wa mwombaji na kuambatisha:-
Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo. Ufupisho wa taarifa za mwombaji (01).
Kivuli cha cheri cha kuzaliwa.
Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
Aidha, inasisitizwa kwamba:-
  • Waombaji wawe na umri kati ya mlaka kati ya 18 na 44
  • Waombaji wa kazi toka maeneo husika na wenye sifa zilizoainishwa katika tangazo hili, watafikiriwa kwanza na kupangiwa kazi katika maeneo husika.
  • Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.
    Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa sasa.
  • Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
  • Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE wakishindwa kutekeleza hili maombi yao hayatashughulikiwa.
  • Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu.
  • Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.
  • Waombaji waliowahi kufukuzwa kazi wasiombe.
  • Waombaji wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia masharti yaliyotajwa hapo juu maombi yao hayatashughulikiwa.
  • Waombaji watakaotoa taarifa za uongo mfano kuhusu umri wao, elimu yao au sehemu walizowahi kufanyia kazi na ikagundulika hata kama watakuwa wameshaajiriwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Application Instructions:

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania,
S.L.P. 8391, DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;-
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P8391,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

0 on: "JOB VACANCY IN ACCOUNT ASSISTANCE AT TGS C,"