Wabunge wa vyama vinavyounda Ukawa jana walisusia futari
iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ikiwa ni mwendelezo wa
hatua za kususia shughuli zote zinazoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia
Ackson.
Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Riziki Ng’wale,
alisema wamechukua hatua hiyo kutokana na Dk Tulia kuwa mgeni rasmi wa
shughuli hiyo.
“Dk Tulia ndiye mgeni rasmi katika shughuli hiyo ya kufuturisha
na sisi tumeamua kuwa hatutashiriki shughuli yoyote inayoongozwa naye,” alisema muda mfupi baada ya kutoka katika kikao cha wabunge wa kambi hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alisema wamekubaliana
wabunge wote wa kambi ya upinzani waliofunga watakwenda kufuturu
majumbani kwao.
“Tumekubaliana hatutakwenda kufuturu bungeni na kila mbunge atakwenda kufuturu nyumbani kwake,” alisema.
Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha wapinzani kilichoketi chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia.
Futari hiyo ilitangazwa na Dk Tulia tangu juzi na kusisitizwa jana
baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa mchana kuwa ingefanyika kwenye
viwanja vya Bunge ambako wabunge wote walialikwa.
Kwa siku zaidi ya 10 sasa, wabunge hao wamekuwa wakisusa vikao vya
Bunge vinavyoongozwa na Dk Tulia kwa sababu hawana imani naye.
Hali hiyo imefanya bajeti kuu kwa ya Serikali kwa mwaka wa fedha
2016/17 kuchangiwa na wabunge wa CCM tu baada ya Dk Tulia kuongoza vikao
kila siku, akiingia asubuhi na jioni
0 on: "HATIMAE Wabunge UKAWA Wasusa Futari ya Waziri Mkuu"